Mavunde atangaza Neema kwa Mafundi Dodoma

 

 MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameahidi kuwatafutia fursa za kandarasi mafundi wa Dodoma kushiriki katika ujenzi wa Jiji la Dodoma unaoendelea kwa kasi hivi sasa.

Mavunde ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na Mafundi zaidi ya 1000 wa Dodoma ambao walikuwa wameandaliwa mafunzo ya ufundi kutoka Kampuni ya Magic Builders International Ltd

Amesema, atahakikisha anawasimamia na kuwaongoza kuifikia fursa hiyo ili nao wawe sehemu ya uendelezaji wa Jiji la Dodoma.

“Sheria ya manunuzi ya umma inataka Taasisi nunuzi kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake kwa ajili ya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu,hivyo nitahakikisha nasimamia kwa dhati ili kupitia umoja huu nanyi muwe wanufaika, ” amesema

Amesema, anataka wajenge umoja wa mafundi utakaozingatia uadilifu,uaminifu na uweledi.

“Kwa kuanzia nitawasaidia kupata ofisi na kuwalipia kodi kwa mwaka mmoja sambamba kuwapatia vitendea kazi vya ofisi,” amesema Mavunde

Akizungumza kwa niaba ya mafundi Dodoma, Twalib Ibrahim amemshukuru Mavunde kwa kukubali kuwa Mlezi wao na pia kwa misaada mbalimbali ambayo amenuia kusaidia mafundi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments