Minziro yamemkuta huko

MBEYA: Klabu ya Tanzania Prisons imemfuta kazi kocha, Fred Felix Minziro kuanzia leo Novemba 21, 2023.
Taarifa iliyotolewa na timu hiyo imeeleza kuwa maamuzi hayo ni kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kocha huyo alijiunga na Prisons mwezi Julai mwaka huu akichukua nafasi ya kocha, Mahamed Bares aliyetimkia Mashujaa Fc ya Kigoma.
Ndani ya miezi minne aliyokinoa kikosi hicho ameiongoza katika michezo tisa ya ligi kuu akishinda mchezo mmoja pekee, amepoteza michezo minne na kutoa sare michezo minne huku akivuna alama saba na ameiacha timu hiyo katika nafasi ya 14 kwenye msimano wa ligi.
Timu hiyo imesema kuwa kwasasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Shabani Mtupa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments