Miroshi awaangukia Watanzania

 

DAR ES SALAAM: Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa stars’, Novatus Dismas Miroshi amewaangukia wapenda soka akijutia kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kusaka kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 dhidi ya timu ya taifa ya Morocco ambao Taifa Stars ilipoteza mabao 2-0.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Miroshi amesema licha ya kupoteza jana bado anaamini Tanzania ina nafasi ya kutamba katika michezo ijayo.

“Nipende kuwaomba radhi wapenda soka wote na Watanzania kwa kupata kadi nyekundu lakini bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri ‘’ ameandika Miroshi.

Kwa matokeo hayo ya jana Taifa Stars imesalia na alama zake tatu ikishika nafasi ya nne kwenye kundi E nyuma ya Morocco, Zambia na Niger wenye alama tatu pia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments