Mkulima jela miaka 20 kwa kukutwa na viungo vya sokwe

JEREMIA Ngendabanka mkulima na mkazi wa Kijiji cha Buhingu, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kupatikana na viungo mbalimbali vya sokwe mtu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Uvinza, Misana Majura Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi, Ephraim Mwakanyamale aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 22, 2022.

Mwakanyamale aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alipatikana na nyara hizo za serikali, ambazo ni mkono mmoja wa sokwe mtu, kichwa kimoja cha sokwe mtu na ngozi moja  ya sokwe mtu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

Akitoa hukumu hiyo wiki hii,  Hakimu Majura amesema kuwa Mahakama imejiriridhisha pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hilo.

Amesema ametoa adhabu hiyo ili  iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uwindaji haramu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments