Mnyama kifua mbele kwa Mkapa

 

Miamba ya kandanda nchini ,Simba leo watatupa karata yao ya kwanza kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL) watakapowaalika, Asec Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi waliopata katika mchezo wa mwisho dhidi ya Asec Mimosas katika Uwanja wa Mkapa uliopigwa February 13, 2022, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wa hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika (CAFCC).

Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni ambapo mashabiki wa Simba wanasubiri kuona muendelezo wa timu hiyo katika michuano ya msimu huu huku Wakuu wa timu hiyo mara kadhaa wakinukuliwa kuwa dhamira yao ni kuvuka hatua ya robo fainali ambayo wamekuwa wakiishia misimu iliyopita.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments