Rais Samia aagana na Rais wa Romania

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagana rasmi na Rais wa Romania, Klaus Werner leo 19 Novemba Ikulu ya Magogoni jijini Dar es salam, baada ya ziara ya siku nne ya kiongozi huyo nchini.

Ziara ya Rais Werner ilikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kimkakati ikiwemo afya, utengenezaji wa dawa, usindikaji wa mazao ya kilimo, madini pamoja na mbinu za kukabiliana na majanga.

Aidha mazungumzo baina yao yamefikia makubaliano ikiwemo kupatikana nafasi 10 kwa ajili ya Watanzania kusoma Romania katika masomo ya udaktari na ufamasi, na Tanzania kutoa nafasi tano za masomo kwa wanafunzi wa Romania kuja kusoma nchini katika vyuo watakavyochagua wenyewe.

Katika ziara hiyo kumekuwepo na uwekaji wa saini wa hati za makubaliano kuhusu kushirikiana katika masuala ya utafiti wa kisayansi katika kilimo na usalama wa chakula pamoja na kukabiliana na majanga.

Sambamba na hayo wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya kimataifa ya mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo itajadiliwa kwa kina kwenye mkutano wa COP28 unaotarajiwa kufanyika Umoja wa Falme za kiarabu mwishoni mwa mwezi Novemba.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments