RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI,AVUNJA BODI YA TCRA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.

2.Amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait. 

Balozi Massoro anachukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3.Amemteua Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mkeyenge alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Bw. Mkeyenge anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

4.Amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 07 Novemba, 2023.          

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments