RC SENYAMULE AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA YA KILIMO BIASHARA

 


Na Okuly Julius-Dodoma 


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amewataka vijana kuchangamkia fursa za kilimo biashara ili kuinua uchumi wao, kuongeza pato la Taifa na kutatua changamoto ya ajira.

Senyamule ametoa wito huo Novemba 24,2023 jijini Dodoma , wakati akifunga kongamano la siku tatu la kujenga uelewa na kubadilishana uzoefu kwa wadau wa kilimo liloandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Kimasoko katika Kilimo (AMDT).


Amesema watu walikuwa wakiongelea kilimo kwa dhana tofauti kuwa wanaofanya shughuli hizo ni maskini lakini ukweli ni kwamba kutokana na mapinduzi yaliyofanyika katika sekta hiyo kilimo ni utajiri.


“Katika hizi siku tatu mlizokaa hapa mtoke na maadhimio ambayo yatawawezesha wananchi wetu wanaojihusisha na shughuli za kilimo kuwa na uratibu wa pamoja,"


Na kuongeza kuwa:”Tunataka kundi kubwa la vijana liingie katika kilimo kwasababu huko kuna utajiri, watainu vipato vyao, wataongeza pato la taifa na kututa changamoto ya ajira kwasababu watajiajiri na kuajiri wengine.


Katika hatua nyingine Senyamule, amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa utashi wake na kuweka nguvu kubwa katika sekta ya kilimo.


Amesema katika uongozi huu wa serikali ya Awamu ya Sita imebadili sekta ya kilimo na kuwa chanzo cha uchumi wa Mtanzania 





“Namshukuru Rais Dk.Samia kwasababu ya utashi wake ambao unafanya sekta ya kilimo inaendelea kuimarika siku hadi siku. Watu walikuwa wakiongelea kilimo kwa dhana ya umaskini lakini sasa hivi kila mtu anatamani kufanya kilimo kwani utajiri upo hukom”amesema Senyamule 


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa AMDT Charles Ogutu, alisema, kongamano hilo limehusisha wadau kutoka katika sekta mbalimbali za maendeleo lengo ni kujifunza na kubadilisha uzoefu.


Amesema kongamano hilo pia lilihusisha wadau maalumu ambao wanahusika na kukopesha fedha na vifaa kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuinuka na kufanya kilimo chenye tija.


“Wadau wamekubaliana kuwa na mikakati ya kujisimamia wwenyewe kwasababu tunamini kuwa tunaweza kufanya mambo makubwa zaidi. Baada ya kutoka hapa kila mtu atatumia kile alichojifunza na kuingiza katika mpango mkakati wake,"ameeleza Ogutu


Naye Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa AMDT Dk.Mary Shetto alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wamefikia wakulima zaidi ya 100,000 katika mikoa mbalimbali


Amesema wameweka kipaumbele katika uzalishaji wa zao la alizeti kwasababu ndio zao ambalo serikali inatumia fedha nyingi kuagiza mafuta nje ya nchi.


“Lengo la kuweka nguvu kubwa katika uzalishaji wa zao la alizeti ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kukidhi mahitaji na kuepuka uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi,”amesema Shetto


MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA UKAGUZI WA MABANDA YA WATAALAMU WA KILIMO NA WAUZAJI WA VIFAA MBALIMBALI VYA KILIMO.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments