Samia atajwa ushindi Taifa Stars

 RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amesema mafanikio ya timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yamechagizwa na hamasa inayotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo alipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kuipokea Taifa Stars, iliyowasili nchini ikitokea Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 dhidi ya Niger hapo jana na kuibuka na ushindi wa 0-1.

Karia amesema Rais ametoa ndege kuisafirisha Stars, hali inayowafanya warejee nyumbani kwa wakati, na kupata muda wa kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 21, 2023.

Kwa upande mwingine, Karia amesema kutokana na mazingira rafiki ya kinchi na hali nzuri za viwanja nchini, Tanzania inapokea timu nyingi za taifa zikitumia viwanja vilivyopo kama viwanja vyao vya nyumbani.

“Kama ulikuwa hufahamu, mpaka sasa kuna timu tano za taifa zipo hapa nchini, ikiwemo Burundi, Gambia, Gabon, Ivory Coast pia Morocco.” Amesema Karia

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments