SERIKALI KUENDELEA KUTOA MIKOPO NA RUZUKU KWA WANAFUNZI WA VYUO.

Na   Mwandishi Wetu RAFURU KINALA.

Serikali imesema itaendelea kutenga Fedha kwa ajili ya kuhakikisha inatoa Mikopo na Ruzuku kwa Vyuo vya Elimu ya Kati na Juu ili kuwezesha Mazingira Bora ya kujifunza na kufundishia, na kuleta tija kwa Wanafunzi wa Vyuo hivyo.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba SULEIMAN MWENDA, akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA alisema hayo katika Mahafali ya 21 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania - TIA Mkoani Singida, ambapo kwa Tawi la Singida ni Mahafali ya 12. 

Alisema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Mazingira ya Vyuo vya Elimu ya Kati na Juu vinatoa Elimu bora.

Mwenda alisema, serikali pia imeendelea kutenga Bajeti kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo ili kuondoa changamoto kwa wanafunzi kwa kutoa Mikopo na Ruzuku.

Aidha Mwenda alitoa wito kwa wahitimu hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maendeleo na kuachana na yale ambayo hayana faida kwao na Jamii.

Awali akizungumza katika Mahafali hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania - TIA Prof. WILLIAM PALANGYO aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Taasisi hiyo kwa kutoa Mikopo kwa wanafunzi.

Prof. Palangyo alisema kumekuwa na ongezeko la wanafunzi katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania kutoka na serikali kuweka mfumo wa elimu bila malipo kwa ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari.

Kwa upande wake Wakili SAID CHIGUMO  ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania - TIA, alitoa wito kwa wahitimu wahitimu hao kuitumia elimu waliopata chuoni hapo kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Wakili CHIGUMO alisema elimu ni moja ya nyenzo muhimu endapo itatumika vizuri, na hivyo wakaitumie elimu hiyo katika kuanzisha shughuli mbalimbali za Kiuchumi.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments