Simba waja kivingine zaidi

 Ofisa  Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Imani Kajula amesema klabu hiyo imedhamiria kuendelea kuiteka mitandao ya kijamii ndio maana leo Novemba 14, 2023 wamezindua chaneli ya Whatsapp ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa taarifa za timu hiyo.

Kajula amesema kutokana na nguvu ya mtandao huo na urahisi wake wameshawishika kuwa miongoni mwa timu zinatakazotumia mtandao huo uliopakuliwa na watu zaidi ya bilioni mbili ulimwenguni kote.

“Leo tumezindua Simba Sports Club WhatsApp Channel, imepakuliwa na watu bilioni 2.2 duniani na ndio mtandao umepakuliwa zaidi duniani,WhatsApp wenyewe walitutafuta kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na channel hii.

“Ni timu chache kama Kaizer Chiefs, Al Ahly, Barcelona, Real Madrid na Simba tumejiunga, katika kuijaribu kabla ya kuzindua ndani ya wiki. Tumepata wafuasi 100,000 ,faida kubwa ni kwa mashabiki kupata taarifa na wadhamini wetu kuonyesha bidhaa zao,” amesema Kajula

Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema klabu hiyo ni wafalme katika matumizi ya mitandao ya kijamii na safari hii wamepania zaidi.

“Katika maeneo yote ya mitandao ya kijamii Simba tumekuwa tukifanya vizuri na leo tumezindua mtandao mwingine na itakuwa na faida kubwa kwa mashabiki. Tunafahamu urahisi wa kutumia WhatsApp kwa hiyo hii itakuwa njia rahisi ya kufikia watu wengi, kuna wengine hawatumii Instagram wala Facebook lakini wana WhatsApp,” amesema Ahmed Ally

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments