Taifa Stars waoga noti za Samia

RAIS Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya kuipatia timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Sh milioni 10 kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger Jana.

Pesa hizo zimewasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wakati wa kuipokea timu baada ya kuwasili leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

“Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais aliahidi kwamba kwenye safari ya taifa stars kila goli atakuwa anatoa Sh milion 10” amesema Msigwa

Pamoja na hilo Rais Samia amelipia eneo la mzunguko lenye takriban viti 30,000 kwajili ya Watanzania watakao fika kuishangilia timu ya taifa siku ya jumanne Novemba 21 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum iitwayo “oparesheni Samia Kombe la Dunia” kwajili ya kuhamasisha timu Kushiriki kombe la dunia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments