Ukurasa mpya mitaa ya Msimbazi

DAR ES SALAAM; Vikao vimeendelea kutawala ndani ya Klabu ya Simba kutokana na matokeo yasiyoridhisha ndani ya timu hiyo.

Novemba 26, 2023, Uongozi wa klabu hiyo ulifanya kikao na wachezaji kufanya tathimini ya kile kinachoendelea ndani ya timu ambapo baada ya kikao hicho wachezaji pamoja na viongozi wamekubaliana kuwa na mwanzo mpya ili kuijenga Simba mpya.

Ikumbukwe Simba hawajapata ushindi katika michezo mitatu mfululizo waliyoshuka dimbani wakipoteza mabao 5-1 kwa watani zao Yanga sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo na mchezo wa watatu wakitoa sare ya 1-1 dhidi ya Asec Mimosas katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo tayari wababe hao wa mitaa ya Msimbazi Dar es Salaam, wamemtangaza kocha Abdelhak Benchikha kuwa mchora ramani mpya ndani ya timu hiyo, ambapo amepewa imani kubwa na mashabiki wa Simba wakiamini atawavusha katika safari yao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments