Ummy atoa siku 7 kupata ripoti kifo cha mjamzito na kichanga

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) kuhakikisha ndani ya siku 7 wamempelekea taarifa ya tukio la kifo cha mjamzito na kichanga chake kilichotokea  Novemba 11 ,2023 mkoani Tanga.

Amesema, tayari hatua za awali zimeshachukuliwa ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kutuma timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha madaktari bingwa wawili akiwemo daktari bingwa wa wanawake na uzazi na daktari bingwa wa huduma za usingizi ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Hatua nyingine iliyochukuliwa baada ya tukio hilo ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuwasimamisha kazi watumishi watatu walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hili baya na lisilopaswa kuvumiliwa.” Amesema Waziri Ummy

Pia Waziri Ummy amewahakikishia Watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi, kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua kali za kitaaluma, kiutumishi na kijinai ikiwemo kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika.

Waziri Ummy ametoa pole kwa familia iliyoguswa na msiba huu na ameahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya ili kufikia matarajio ya wananchi wote.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments