VETA SINGIDA WAISHUKULU SERIKALI KWA KUENDELEA KUJENGA VYUO VYA VETA NA KUFADHILI MAFUNZO.

                 

Mkuu Chuo cha Ufundi Stadi - VETA Singida, ALPHONSINA MSHANA ameishukuru serikali kwa kuendelea Kujenga Vyuo vya VETA kila Wilaya nchini na kufadhili mafunzo kwa wanafunzi ili kutatua changamoto ya Ajira kwa Vijana, kwa kujiajiri wenyewee mara baada ya kupata Mafunzo katika Vyuo hivyo.


ALPHONSINA alisema hayo katika Mahafali ya 34 ya Chuo cha VETA Singida, ambapo alisema serikali imeendelea kutatua changamoto mbalimbali katika vyuo vya VETA ili kuweka mazingira rafiki ya kujifunza na kufundishia.

Alisema Chuo hicho kimekuwa mkombozi kwa Vijana na Jamii kwa Ujumla wanapohitimu katika Vyuo hivyo kwani hupata ujuzi ambao huwasaidia kujiajiri wenyewee au kuajiriwa Serikalini na Taasisi mbalimbali.

ALPHONSINA alisema pia Chuo hicho kwa sasa kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa vifaa vinavyoendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Alisema VETA Singida bado wanatumia Vifaa vilivyopitwa na wakati na hivyo kuwapa wakati mgumu wahitimu wanapokutana na Vifaa vya kisasa vinavyoendana na Teknolojia ya sasa katika maeneo yao ya kazi.

Akisoma Risala kwa niaba ya wahitumu Rais wa Chuo cha VETA Singida SAMWEL SPYRIAN, alisema kupitia mafunzo waliyoyapata Chuoni hapo yatawasaidia kujiajiri wenyewe na hata kuajiriwa Serikalini au Taasisi mbalimbali.

SPYRIAN aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutatua Changamoto ya Ajira kwa Vijana, kwa kuanzisha Miradi na Mafunzo mbalimbali ya kuwakwamua vijana Kiuchumi.

Akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha VETA Singida, Mkwakilishi wa Kiwanda cha Pamba Singida, EDWARD JOSEPH alitoa wito kwa Wahitimu kuhakikisha wanakuwa na maadili mzuri katika Jamii.

JOSEPH alisema wakiwa na Maadili mema katika Jamii itawasaidia wahitumu hao kuaminika katika kazi zao.





Na RAFULU KINALA  SINGIDA.


             

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments