Waandishi 6 wapewa tuzo habari za sayansi

TAASISI ya Sayansi Afrika (SFA), imetoa tuzo kwa waandishi sita waliofanya vizuri katika kuandika habari za kisayansi.

Hafla ya kuwatangaza washindi hao ilifanyika Lusaka, Zambia unakofanyika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2023).

Meneja Mawasiliano wa Biashara na Sayansi SFA, Debora-Fay Ndlovu amesema hayo muda mchache kabla ya kutangazwa kwa washindi hao.

Amewataja washindi hao kuwa ni Laura Grant kutoka Afrika Kusini, Mary Mwenda (Kenya), Mahmud Mohammed (Ghana), Jean Pierre (Rwanda), Ridwan Karibu (Ghana) na Josephine Chinele (Malawi).

Akitoa shukrani zake Pierre amesema amefurahi kushinda tuzo hiyo ya uzinduzi kwa kuwa juhudi zake zimetambulika.

Amesema atatumia ujuzi wake katika kuandika habari zaidi za kisayansi zinazoelimisha na kuwafahamisha watunga sera, jumuiya ya wanasayansi, wananchi na jamii kwa ujumla.

Naye Laura Grant amesema,“Tunajivunia kupokea tuzo hii ya uzinduzi. Kuna utafiti mwingi bora sana ambao wanasayansi katika bara la Afrika wanafanya ambao hauandikwi kwenye kwenye vyombo vya habari,” amesema.

Ameleza kupitia tuzo hizo ataendelea kuandika habari za kisayansi ambazo wakati mwingine ni ngumu kuziweka katika lugha rahisi ili wananchi waweze kuzielewa. Maombi 204 ya kuwania tuzo hizo kutoka nchi 17 za Afrika yalitumwa na kuchujwa.

Nchi ambazo waandishi walituma maombi hayo ni Benin, Burkina Faso, Cameroon, Misri, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Malawi, Morocco, Nigeria, Uganda, Tanzania, Tunisia, Sudan, Afrika Kusini, Rwanda, Zimbabwe

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments