Wahitimu TIA watakiwa kuangalia changamoto za jamii

WAHITIMU wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) kampasi ya Mwanza wameshauriwa kujiendeleza kielimu pamoja na kufanya utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.

Ushauri huo umetolewa leo na Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya wakati wa mahafali ya kwanza ya taasisi hiyo yaliofanyika katika viwanja vya taasisi wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Balandya amewataka pia wahitimu kutumia elimu walionayo kupambana na umaskini pamoja na kujiajiri ili waweze kuleta mabadiliko katika jamii.

Ameiagiza taasisi ya uhasibu tawi la Mwanza kuandaa wahitimu watakaoweza kuajirika na kujiajiri. Balandya ameipongeza Serikali kwa kuweza kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ya juu.

Amewaagiza wahitimu wanawake kuhamasisha wanawake wenzao kuweza kujiunga na Elimu ya juu.

Naye mkuu wa Taasisi ya Uhasibu nchini Profesa William Pallangyo amesema mahafali hayo ni mahafali ya kwanza kwa kampasi ya TIA Mwanza na ni mahafali ya 21 kwa kampasi zote za uhasibu nchini. Amesema katika mahafali ya Mwanza wamehitimu wanafunzi 947 ambapo wanaume ni 421 na wanawake ni 526.

Amesema mkakati wa elimu bila malipo umesaidia sana kuongeza udahili wa wanafunzi. Amesema katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa mkopo kwa wanafunzi 540.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments