Wanachama 20 CCM wawania uwenyekiti Arusha

 


WANACHAMA na makanda maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 20 mkoani Arusha wamejitokeza kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya mkoa iliyoachwa wazi na Zellothe Stephen Zellothe aliyefariki dunia.

Zellothe alifariki Oktoba 26 mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili iliyopo jijini Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Fomu za kuwania kiti hicho ngazi ya mkoa ilitangazwa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mussa Matoroka na uchukuaji na urudishaji wa fomu hizo unatarajiwa kufungwa kesho Novemba 23 mwaka huu majira ya saa 10 jioni.

Miongoni mwa waliochukua fomu ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mstaafu Lootha Sanare ambaye pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Monduli kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo ngazi ya mkoa kwa kumwangusha Michael Lekule Laizer na baadae kuchaguliwa kuwa Mkuu  wa Mkoa wa Morogoro.

Mfanyabiashara Maarufu wa kusaga nafaka Arusha Philemoni Mollel maarufu kwa jina la Monaban,Mussa Mkanga diwani mstaafu wa chama hicho kata ya Sombetini na Daniel Pallangyo aliyewahi kuwa MNEC wa mkoa ni miongoni wa mwa makanda wa CCM Mkoa wa Arusha waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ngazi ya mkoa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments