WANAOMKANA HAYATI MAGUFULI RAIS SAMIA ANAWATAZAMA ANAJUA IPO SIKU MTAMKANA NA YEYE – MWENEZI MAKONDA

 

“Mimi ni muumini wa kutambua chanzo cha baraka, kama hutambui chanzo chako cha baraka zako zimeanzia wapi basi atakayekupa baraka kwasasa bado hutomshukuru, ni vema kushukuru na kutambua baraka ulizopewa”

“Wanasiasa wenzangu niwaambie tu ukweli msisahau watu waliowashika mikono, wapo watu wanamsema vibaya Hayati Magufuli na kumsahau mema aliyowatendea na watu kama hao maana yake siku moja watakuja kusahau mema wanayotendewa na Rais Samia”

“Rais Samia ni Mama mwenye hekima na busara kubwa mno, anatumia sana akili na anawaangalia tu mnaomkana Hayati Magufuli anajua ipo siku mtamkana na yeye kwahiyo kuweni na upendo wa kweli, Chama Cha Mapinduzi kimetulea na kutufunza naamini hatujafunzwa kuwa wanafiki.”

Paul Makonda
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa amezungumza hayo na Wananchi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza kwenye ziara yake leo tarehe 12 Novemba, 2023.   


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments