WANAWAKE KUPEWA KIPAUMBELE KWENYE BIASHARA ILI KUKUA KIUCHUMI




Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WANAWAKE Wafanyabiashara na Wajasiriamali wameendelea kupewa kipaumbele kwenye majukwaa mbalimbali ya biashara na ujasiriamali ili kuhakikisha wanapata maendeleo na kukua kiuchumi kupitia shughuli hizo za biashara na ujasiriamali.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila kwenye Kongamano la Maandalizi na Masoko kwa Wanawake na Vijana Wajasiriamali lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhe. Chalamila amesema taifa la Tanzania limeendelea kuandaa na kuratibu sera mbalimbali za kuwawezesha Wanawake na Vijana wanafurahi na kupata maendeleo kupitia biashara hizo.

“Dar es Salaam tumekuwa na kipaumbele kikubwa kutoa fursa za biashara kwa wanawake ili kuwafanya kukua na kupata maendeleo kupitia biashara hizo na ujasiriamali,” amesema Mhe. Chalamila 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Chember of Commerce (TWCC), Mwajuma Hamza alisema wanatoa mafunzo hayo kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake katika majukwaa makubwa ili Kuwawezesha kuyafikia na kupata mafanikio ili kukua kiuchumi na kupata maendeleo.

“Wanawake hajalala wanaendelea kuchangamkia fursa zaidi kwenye majukwaa mbalimbali ili kufikisha biashara zao ili zikue, sisi TWCC tunaendelea kuhamasisha zaidi hata wale Wanawake Wafanyabiashara wa mikoani ili na wao wachangamkie fursa hizi zilizopo,” amesema Mwajuma.

Vile vile, baadhi ya Wanawake Wafanyabiashara na Wajasiriamali mbalimbali wameshukuru TWCC kuwapa mafunzo hayo kupitia Kongamano hilo la Wanawake na Vijana hususani kushiriki kwneye majukwaa makubwa ya fursa za biashara ili kupeleka biashara hizo na kukua kimaendeleo na kukua kiuchumi kiujumla.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments