Ajali ya Hiace yaua 4, yajeruhi 21

 

KAGERA; Bukoba. Watu wanne wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa katika ajali iliyosababishwa na gari lenye usajili namba T 339 DBV aina ya Toyota Hiace, iliyokuwa ikitokea Izimbya Bukoba Vijijini kuelekea Bukoba Mjini mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa tano asubuhi leo Desemba 5, 2023, maeneo ya Kyetema katikati ya Kata za Kemendo na Bujugo Halmashauri ya Bukoba.

Kamanda Chatanda amesema waliopoteza maisha ni watu wazima watatu na mtoto mmoja, huku kati ya majeruhi 21 watoto ni 4 watu wazima 17, ambao walikimbizwa Hospitali ya Bujuna Ngoma ambayo ni ya wilaya hiyo.

Hata hivyo amesema kutokana hali ya majeruhi wengi kuwa mbaya, wengine wamehamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi dereva aliyeshindwa kulimudu gari kwenye mteremko likaenda kugonga nguzo za umeme pamoja na pikipiki zilizokuwa kwenye maegesho ya barabara.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments