Ajali yaua wawili na kujeruhi 50 Pwani

Watu wawili wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa miezi sita na wengine hamsini kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya basi ndogo aina ya tata liliokuwa inatoka Kigogo Dar es Salaam kuelekea Mloka Rufiji kupitia njia ya Kisarawe kupinduka na kutumbukia mtoni.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alipofika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kuwapa pole na kuwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya Kisarawe amethibitisha vifo vya watu hao na kupokea idadi ya majeruhi 50 ambao kati yao saba wamekimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya majeruhi walionusurika katika ajali hiyo akiwemo mama mzazi aliyefiwa na mwanae wameeleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi wa dereva.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ilihusisha gari lenye namba za usajiri T.275 DRZ iliyokuwa ikitokea Kigogo kwenda Mloka Rufiji.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments