BILIONEA wa Uingereza, Jim Ratcliffe amekubali kununua hisa asilimia 25 za Manchester United kwa takriban Dola bilioni 1.3.
Taarifa ya BBC Sport imeeleza tajiri huyo mwenye umri wa miaka 71 pia atatoa Dola milioni 300 ambazo sawa na pauni 236 kuwekeza uwanja wa Old Trafford hapo baadaye.
Tangazo hilo linakuja miezi 13 baada ya wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer, kusema wanafikiria kuuza ili kutafuta mbinu mbadala. Familia hiyo ya Marekani ilinunua klabu hiyo kwa Pauni milioni 790 mwaka 2005.
Mzabuni mwingine pekee aliyetangazwa hadharani, mwanabenki wa Qatar Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani, aliondoa ofa yake ya kununua 100% ya klabu mnamo Oktoba mwaka huu.
United wamekuwa na mwenendo usio mzuri kwa miaka ya hivi karibuni hawajashinda Ligi Kuu tangu 2013, huku mashabiki wakiandamana mara kadhaa kushinikiza kuondoka kwa familia ya Glazer ambao ndio wamiliki wa klabu kwa sasa.
0 Comments