CHATANDA ALIA KWA UCHUNGU MARA BAADA YA KUKUTANA NA MAMA MJAMZITO ALIESOMBWA NA MAFURIKO HANANG KISHA KUOKOLEWA NA HATIMAE KUJIFUNGUA SALAMA

                    

Mwenyekiti  wa Umoja wa wanawake  Tanzania UWT, Mary Chatanda  na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona  Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuonea mwili mzima  na kumsomba mita kadhaa.


Akizungumza jana alipomtembelea Mwanamke huyo katika  Kituo cha Afya Gendabi mahali  ambapo ndipo kulikuwa  na Maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada  ya Mlima Hanang kupasuka.

"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama  huyu ambaye  alisombwa na tope na kuweza kuokolewa  kwenye tope hilo  na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua  salama

Mtoto wa kiume  3/12/2023 kwa kweli nimelia uchungu  baada ya kusikiliza  simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama . Namshukuru  sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha Mama huyu kujifungua  salama na mtoto yupo Salama  na ameitwa Mussa ." 

Aidha Mwenyekiti  amesema  Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea  mahitaji ya kutosha 
Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba  baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang .

Chanzo UWT Taifa



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments