HABARI PICHA KUTOKA POLISI MKOA WA SONGWE

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP. Theopista Mallya Desemba 03, 2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Mapadre Parokia ya Mtakatifu Hellena Jimbo kuu la Mbeya kwa Paroko Isaya Nyambo lililopo Igamba Wilayani Mbozi.


Kamanda Mallya akiwa kama mgeni rasmi katika harambee hiyo aliwezesha kuchangisha kiasi cha shilingi Milioni 3 na Laki Tano kwaajili ya kununua mbao za kupaulia jengo hilo ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.

Sambamba na harambee hiyo Kamanda Mallya alipata nafasi ya kuzungumza na waamini wa Kanisa hilo na kuwataka waamini hao na jamii nzima kukemea vitendo vya RUSHWA pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, pia kukemea vitendo vilivyo kinyume na Mila na Desturi za Taifa letu,hasa vinavyosababisha ukatili dhidi ya watoto.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments