Kinana akemea vitisho, majungu, mizengwe Bukoba

KAGERA: MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amekemea majungu, fitina, mizengwe na vitisho kwa wanaozuia miradi ya kimkakati.

Kinana ameyasema hayo leo Desemba 11, 2023 baada ya kutembelea miradi ya kimkakati ambayo ni stendi ya mabasi, ujenzi wa barabara nne na soko mjini Bukoba mkoani Kagera.

Baada ya kukagua miradi hiyo amekutana na kuzungumza na wazee wa mkoa huo ambapo Mwenyekiti wa Wazee Bukoba, Joseph Masabala akizungumza kwa niaba ya wazee alilalamikia kukwama kwa miradi hiyo ya maendeleo kwa kile walichadai ni ubinafsi unaofanywa na watu wachache na kusababisha wananchi kuishi maisha ya tabu.

Akizungumza na wazee hao Kinana amesema “Kuna mambo matatu muhimu ambayo wananchi wakishirikishwa vizuri hali itakuwa nzuri, ila wasiposhirikishwa hali itakuwa mbaya.

“Kagera ni miongoni mwa mikoa michache ambayo haina barabara nne, maendeleo yanagharama, baadhi ya nyumba na maduka ni lazima ziondoke kupisha ujenzi wa barabara,” amesema.

Aidha, amesema Kagera ni Mkoa wenye biashara, una ardhi nzuri yenye rutuba, wasomi wa kutosha wakiwemo maprofesa 666, lakini ni mmoja wa mikoa yenye mapato madogo zaidi.

“Kila kitu mnacho kwa nini mapato ya mkoa huu yapo chini kuliko mikoa yote? alihoji.

Pia, Kinana amekemea tabia ya wanasiasa wa Kagera kujifungia badala ya kutoka kwenda kwa wananchi na kuwashawishi kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kinana amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Mungu akimjalia atahudumu kwa miaka minane, uhai wa taifa ni mkubwa kuliko uhai wa mtu, amefanikiwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo maji, elimu, umeme, barabara katika mikoa yote kwa asilimia 80 hakuna mradi ambao upo chini ya asilimia hiyo.

“Sasa nyie endeleeni kutisha, endeleeni na fitina, majungu, Rais Dk. Samia atakapokuja hapa akiuliza barabara ya njia nne mseme mpo kwenye mchakato, soko tupo mbioni, stendi tupo kwenye mazungumzo…

“Msikubali wachache wazuie maendeleo ya wananchi, waswahili wanasema umoja ni nguvu, msemo mwingine unasema wingi si hoja, chagueni wenyewe wingi si hoja au umoja ni nguvu, niwashauri…shikamaneni muwe kitu kimoja, acheni kutengeneza makundi, huyu hafai, acheni kupoteza muda kujadili watu jadilini hoja, kutengeneza mizengwe ni kurudishana nyuma,” amesisitiza.

Akizungumzia vitambulisho vya NIDA, Kinana amesema ni muhimu kwa wananchi kufuata utaratibu kupata vitambulisho hivyo kuepuka usumbufu.

“Kagera ni mkoa ambao upo mipakani na mipakani kuna mambo mengi, kila nchi ina taratibu zake, sasa kama wewe ni raia halali kwa nini usifuate taratibu, msiwafiche ambao sio raia, viongozi ms

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments