Masau Bwire ajinadi JKT Queens ubingwa tena

 

Mara: AFISA Habari wa JKT Queens, Masau Bwire amejinadi kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, dhidi ya Bunda FC, utakaopigwa katika Uwanja wa Karume mjini Musoma, Mkoa wa Mara.

Akiwa mjini Musoma, Bwire amesema katika mchezo wa leo wa ufunguzi wa ligi hiyo msimu wa 2023-2024, JKT Queens imedhamiria kutetea ubingwa wake.

“Wadau, wapenzi na mashabiki wa soka katika mji wa Musoma na maeneo Jirani, wamekuwa wakituona katika luninga, waje watushuhudie.” amesema Bwire.

Nyasi za viwanja vingine vitatu vitatumika katika michezo ya ufunguzi wa ligi hiyo leo, ambapo Simba Queens vs Ceasiaa Queens (Uwanja wa Azam complex jijini Dar es Salaam), Alliance Girls vs Geita Queens (Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza) na Fountain Princess vs Amani Queens (Uwanja wa Jamhuri, Makao Makuu ya Nchi, Dodoma).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments