Mashirika ya hisani yaonywa ufichaji taarifa

MASHIRIKA ya dini na yake yasiyo ya kiserikali yanayoishughulisha na kusaidia watu wenye uhitaji yametakiwa kuweka wazi taarifa zao za mapato na matumizi hasa fedha wanazoomba kwa wahisani ili kuwasaidia wenye mahitaji.

Mkuu wa Wilaya Kigoma, Salum Kali alitoa kauli hiyo alipohudhuria hafla ya Taasisi ya Kigoma Community for the Poor (KPC) ilipokuwa ikikabidhi zawadi za nguo za sikukukuu za mwisho wa mwaka na zawadi nyingine kwa wazee wanaoishi kwenye makazi ya wazee SILABU Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kali alisema kuwa ipo tabia ya baadhi ya mashirika ambayo yanaomba na kupata fedha nyingi kutoka kwenye mifuko mbalimbali ya hisani ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia wasiojiweza lakini misaada inayotolewa kwa walengwa ni kiasi kidogo ukilinganisha na walichopewa kwa kazi hiyo.

Alisema kuwa ni lazima viongozi wa mashirika wawe na moyo wa kibinadamu badala ya kutumia mgongo wa masikini kujinufaisha ambapo ameipongeza KPC kwa kazi kubwa na nzuri ya kusaidia makazi ya wazee wasiojiweza SILABU kwa misaada mbalimbali ikiwemo mishahara ya baadhi ya watumishi wa kituo hicho.

Awali Katibu wa KPC,Mchungaji Ludo David  akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya Kigoma alisema kuwa jumuia hiyo kupitia mashirika mbalimbali 20 kama wanachama  imekuwa ikisaidia kambi hiyo ya wazee kwa miaka 20 sasa likiwemo Shirika la Joy and The Harvest ambalo linasaidia mishahara ya watumishi kwenye kambi hiyo.

Mchunga David alisema kuwa mwaka huu taasisi hiyo imeweza kulipa Sh milioni 10 mishahara ya watumishi wa kituo,ada za wanafunzi  kiacha cha Sh milioni 1.3, gharama za matibabu kwa wazee na Watoto shilingi milioni 1.2 ambapo katika hafla hiyo wamekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu zenye thamani ya Sh milioni 1.7.

akizungumzia misaada mbalimbali na huduma zinazotolewa kwa wazee hao wa SILABU Katibu wa kamati ya uongozi ya kituo hicho, Veronica Ramadhani ameishukuru serikali inayoendesha kituo hicho na wahisani mbalimbali waakiwemo Joy and the Harvest ambao wamekuwa wafadhili wakuu wa kituo chao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments