Mchengerwa atoa mwezi mmoja Hospitali Muleba ikamilike

KAGERA: WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemtaka Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Dk Peter Nyanja kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Muleba unakamilika kabla ya mwezi Januari, vinginevyo amemuonya atamsimamisha kazi.

 

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera, Mchengerwa ametoa siku nne kwa Mhandisi Zefania Chacha na DED aliyepita na kuhamishiwa Manispaa wilayani Tabora, Elias Kayandabila kutoa maelezo ya kina kwanini fedha zilizotengwa Sh milioni 500 zimeshindwa kukamilisha kazi hiyo.

“Hawa wote wananchi wanataka kupewa huduma. Tumesimama kutoa huduma kutokana na uzembe wa watu wachache, hatuwezi kukubali,” amesema Mchengerwa.

 

Amesema, TAMISEMI  imekabidhi Sh milioni 500 kwa kila Halmashauri isiyo na hospitali ya Wilaya kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje na maabara lakini kutokana na ufadhilifu na usimamizi mbovu umepelekea kuzorota kwa mradi huo na miradi kadhaa nchini.

“Mambo haya ndio yanapelekea sasa tunajenga vituo vya Afya. Tulipaswa tujenge awamu ya kwanza, awamu yapili, awamu ya tatu. Na tukifanya mchezo tutaendelea kujenga mpaka awamu ya tisa na ya kumi.” Amesema Mchengerwa.

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muleba umezinduliwa Mei, 2022 na Mkuu wa wilaya hiyo ambaye ameshahamishwa, Toba Nguvila katika eneo la Marahala wilayani humo ila mpaka sasa bado ujenzi haujakamilika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments