Mexime: Nani kasema Simba ni dhaifu?

 

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema ni kuikosea Simba heshima kusema hawana msimu mzuri kutokana kile wanachokionesha katika michezo mbalimbali.

Mexime amesema watu wengi hawatizami michezo kiufundi ndio maana inakuwa rahisi kusema Simba ni dhaifu.

Amesema Klabu ya Simba inacheza michezo migumu tena ndani ya siku chache kitu ambacho kwake yeye anaamini kinaiongezea timu hiyo ubora na ndipo daraja la Simba na Yanga linapojitenga na timu nyingine.

“Mjue Simba na Yanga wanafaida sana kwasababu wanacheza michezo mfululizo, sisi ambao tunacheza mchezo mmoja baada ya wiki mbili ndio tunaoathirika na wao wanafaidika tuu, ukiwatizama upinzani wanaotoa katika michezo ya kimataifa utanielewa kauli yangu,” amesema Mexime.

Amesema amekiandaa kikosi chake vizuri kupambana katika mchezo utakaoikutanisha timu yake ya Kagera Sugar na Simba kesho Desemba 15 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments