Rais Samia ataka mabadiliko wahitimu vyuo vikuu

ZANZIBAR: RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuleta mabadiliko chanya katika jamii mara wanapohitimu masomo yao.

Ameyasema hayo leo mjini Zanzibar katika Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na kueleza kuwa nimefarijika kuona wanawake wanazidi kuhamasika katika elimu.

“Nimepata faraja kuona asilimia 58 ya wahitimu leo ni wanawake,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD) ya Usimamizi wa Utalii na Masoko ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuinua utalii kabla ya kuwa Rais na hata wakati wa urais kupitia Royal Tour.

“Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa nimesimama mbele ya umma huu kukubali Shahada hii.” Amesema Rais Samia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments