Rais Samia atoa mkono wa sikukuu makundi maalum

TANGA: Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka kwa vituo 14 vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na makazi ya wazee mkoani Tanga

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema zawadi hizo ni kwa ajili kuwakumbuka makundi hayo ili nao waweze kusherehekea sikukuu .

“Rais ametoa zawadi hizo kwa makundi hayo maalum yaliyopo kwenye wilaya nane za mkoa huu ili nao wafurahie sikukuu kama sehemu ya jamii nyingine”amesema RC Kindamba.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa ametoa rai kwa jamii kupenda kutoa mahitaji ikiwemo na kuwajali makundi ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kudumisha amani umoja , upendo na mshikamano.

Jumla ya walengwa 334 waliopo kwenye vituo 14 ikiwemo makazi ya wazee wasiojiweza  yaliyopo Mwanzange jijini Tanga wameweza kupatiwa zawadi hizo

Kila kituo kimepewa mbuzi mmoja , Mchele Kg 50 , Mafuta ya kupikia lita 10 sabuni katoni moja , maharage Kg 10 na sukari Kg 10.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments