Katika mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania bara leo KMC watakuwa wenyeji wa Simba Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia saa 10:00 jioni.
Simba wanaingia katika mchezo huo kwa matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri kutokana na rekodi nzuri waliyo nayo dhidi ya KMC.
Timu hizo zimekutana mara 10 huku Simba wakishinda michezo tisa na kuondoka na sare katika mchezo mmoja hivyo hesabu zinaonesha kuwa Simba rekodi zinawabeba dhidi ya KMC.
Mchezo wa mwisho walipokutana Simba akiwa ugenini alimchabanga KMC mabao 3-1 huku Nahodha, John Bocco akiongoza maangamizi hayo akifunga goli la kwanza katika mchezo huo.
0 Comments