Simba, Yanga mbele kwa mbele Robo Fainali CAF

RAUNDI mbili zilizomalizika za Ligi ya Mabingwa Afrika kimahesabu zinatoa picha ya ugumu wa njia ya Simba na Yanga kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Njia zote mbili zinaonekana ngumu zenye milima, mito, mabonde na miiba migumu, ya Simba ikionekana kuwa nzito zaidi kutokana na ubora wao na ubora wa wapinzani wake kwenye kundi lake.

Katika kundi la Yanga ni wazi kwamba National Al Ahly atakuwa mbabe wa kundi hilo, pengine asipoteze hata mechu moja. Mpaka sasa ni Al Ahly pekee walioweza kuchukua pointi moja ugenini kwenye mechi dhidi ya Yanga. Medeama na Belouzdad kila mmoja amekufa ugenini na kushinda nyumbani.

Hivyo kwa hali iliyopo na kwa ubora wa timu zilizopo kwenye kundi hilo, kuna dalili kubwa kwamba Al Ahly haitapoteza hata mchezo mmoja kwenye kundi lake. Ni timu ambayo ama itaondoka na pointi moja au zote tatu ugenini na hakuna wa kuifunga nyumbani.

Kutokana na hilo Al Ahly ataongoza kundi lake maana atashinda mechi zote za nyumbani na atachukua walau pointi moja au zote ugenini.

Nafasi ya pili inagombaniwa na timu zote tatu, Yanga Belouzdad na Medeama lakini nafasi kubwa ipo kwa Belouzdad au Yanga.

NJIA YA SIMBA KWENDA ROBO FAINALI

Kundi la Simba limechachuka na halitabiriki. Kutokana na viwango vilivyooneshwa katika kundi hilo, Simba ana kazi ngumu ya kuifunga ASEC na Wydad ugenini kwani akishinda mechi mbili za nyumbani dhidi ya Wydad na Jwaneng Galaxy na kupoteza mechi zote za ugenini atafikisha pointi 8 tu.

Kwa hiyo ili avuke pointi nane lazima ahakikishe pamoja na kushinda mechi za nyumbani, anaokota walau pointi moja ugenini dhidi ya Wydad na ASEC. Sio kazi ndogo hiyo! Akiokota moja moja ugenini na akashinda zote nyumbani atafikisha pointi 10, Wydad asipojikaza huenda group hili akaenda Simba na ASEC.

 

In worst case scenario, ataenda ASEC na Waydad lakini in fouvarable case scenario ataenda ASEC na Simba. Jwaneng watabakia tu na makhirikhiri yao huko Botswana.

Yanga anaweza kuchukua pointi moja ugenini dhidi ya Medeama na pointi zote sita nyumbani dhidi Medeama tena na Belouzdad. Kule ugenini kwa Ahly Yanga akijitahidi labda apate pointi moja lakini uwezekano mkubwa atakufa mbele ya Ahly.

NJIA YA YANGA KWENDA ROBO FAINALI

Raundi ya tatu Yanga akichukua pointi moja kwa Medeama halafu Belouzdad akifa kwa Ahly ugenini kundi litakiwa hivi…

1. Al Ahly (7)

2. Madeama (4)

3. CR Belouzdad (3)

4. Yanga Afrika (2)

Raundi ya nne Yanga watakuwa nyumbani Benjamini Mkapa Dar es Salaam na Medeama na Ahly atakuwa ugenini na Belouzdad.

Matokeo ambayo yako most probable ni Yanga kuondoka na ushindi na Belouzdad kushika bomba mpaka mwisho na kuambulia sare na Ahly. Hivyo kundi litakuwa hivi…

1. Al Ahly (8)

2. Yanga Afrika (5)

3. CR Belouzdad (4)

4. Madeama (4)

 

Raundi ya tano Yanga anaikaribisha Belouzdad uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Kisasi ni haki. Lazima Medeama afe na uwezo huo Yanga wanao. Kule Ghana Medeama lazima afe kwa Ahly maana kama Yanga watakuwa wamechukua tatu kama tulivyoona hapo juu, Ahly anazikosaje sasa kwa mfano! Labda awe amerelax na baridi ya kileleni. Kundi litakuwa hivi…

1. Al Ahly (11)

2. Yanga Afrika (8)

3. CR Belouzdad (4)

4. Madeama (4)

Raundi ya mwisho Yanga hata kama atakufa kwa Al Ahly ugenini na Belouzdad akamkanda Medeama nyumbani bado haitabadilisha msimamo. Kundi litamalizika hivi…

1. Al Ahly (14)

2. Yanga Afrika (8)

3. CR Belouzdad (7)

4. Madeama (4)

Kutokakana na uchambuzi huo, Yanga akibugi tu halafu akafungwa mechi na Medeama, shughuli itakuwa imeishia hapo maana kumfunga Ahly nyumbani ni jambo ambalo hata kufikirika halifikiriki.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments