Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilile akisisitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wa EWURA Kanda ya Ziwa ( hawapo pichani) kilichojadili utendaji wa Ofisi hiyo, 7 Desemba 2023
..........
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) , Dkt James Andilie, amesema kuwa, EWURA inaendelea kuboresha mifumo yake ya kieletroni ili kuimarisha upokeaji wa taarifa za shughuli za uagizaji, uhifadhi, usambazaji na uuzaji wa bidhaa hiyo nchini.
Dkt Andilile ameyasema hayo 7 Desemba 2023, alipofanya kikao kazi na watumishi wa EWURA Kanda ya Ziwa, jijini Mwanza na kueleza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuleta ufanisi zaidi katika udhibiti wa sekta ya mafuta na kukidhi kwa ufasaha dhima ya Serikali ya huduma mtandao( e-services).
“ Wote mnafahamu Mamlaka imekuwa ikitumia mfumo wa NPGIS ( National Petroleum and Gas Information System) kupokea taarifa hizi, tumebaini baadhi ya changamoto, kwa sasa tunazifanyia kazi, hivyo nitumie fursa hii pia kuwakumbusha wafanyabiashara, baada ya maboresho haya, hakuna taarifa itakayopokelewa nje ya mfumo”. Alisisitiza
Pia, ameeleza kuwa, EWURA inaendelea na maandalizi ya mfumo wa ATG( Automatic Tank Gauging System) utakaowezesha kupata taarifa ya kiasi cha mafuta katika kila tenki la kuhifadhi mafuta nchini kila siku, wakati wowote kwa njia ya mtandao.
Aidha, amewasihi wafanyakazi wa EWURA kutii kanuni za utumishi wa umma na kuzingatia misingi ya maadili ya EWURA ya kuwa waadilifu, kutenda kazi kwa weledi, ufanisi na utu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina alitumia fursa hiyo kuahidi kuwa, Kanda yake itaendelea kushirikiana na wadau wake kwa uthabiti zaidi kama chachu ya kuboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilile akisisitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wa EWURA Kanda ya Ziwa ( hawapo pichani) kilichojadili utendaji wa Ofisi hiyo, 7 Desemba 2023
Kikao kazi kati ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile na watumishi wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa kuhusu tathmini ya utendaji wa Ofisi hiyo, 7 Desemba 2023
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilile ( kushoto) akisalimiana na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina, wakati kiongozi huyo alipoitembelea Ofisi hiyo kufuatilia utendaji wake, mnamo tarehe 7 Desemba 2023
Watendaji wa EWURA kutoka Makao makuu wakifuatilia utendaji wa Ofisi ya EWURA Kanda ya Ziwa wakati wa ziara ya kikazi iliyolenga kutathmini hali ya utoaji huduma za udhibiti wa nishati na maji mnao tarehe 7 Desemba 2023.
0 Comments