Tanzania bila ajali inawezekana

MWANZA: BAADHI ya maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mwanza wakifanya ukaguzi wa vyombo vya moto sambamba na kutoa elimu ya usalama barabarani ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa aliyo yatoa hivi karibuni katika kuelekea kipindi hiki cha sikukuu.

Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza, askari wa kikosi hicho wameendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto kama mabasi yaingiayo na yaendayo mikoani, magari makubwa ya mizigo, daladala pia bodaboda.

Imeshuhudiwa pia madereva wakipimwa kilevi. Hii yote ni kuhakikisha watumiaji wote wa barabara na vyombo vya moto wanakuwa salama kabla na baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka kumalizika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments