“Tukikubali na kutii tutakula mema ya nchi”

MTWARA: WAKATI Wakristo Tanzania wakiungana na wengine duniani kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa ya Noel, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtwara Mjini, Daudi Nalima amewasihi watanzania na viongozi wanaojiandaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao kuhakikisha wanasimamia haki kulinda amani ya nchi.

Mchungaji Nalima ametoa wito huo leo wakati akiongoza ibada takatifu ya Noel (Krismasi) katika Kanisa kuu la KKKT Mtwara. Amesema Tanzania ni taifa lenye historia nzuri ya kulinda amani hivyo ni vyema amani hiyo ikaendelea kulindwa wakati wowote ikiwemo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ujao na uchaguzi mkuu wa viongozi.

“Ninawasihi katika jina la Yesu Viongozi wetu mnaotutawaka kusimamia haki katika kweli , kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa, na hata uchuguzi mkuu , taifa la Tanzania liwe mfano wa mataifa mengine , liwe mfano kwa mataifa bila kubaguana,” amesema.

 

Akirejea katika maandiko matakatifu ya Mungu (Isaya 1:19), Mchungaji Nalima amesisitiza viongozi kutii na kuzingatia misingi ya kulinda amani ya Tanzania ili kupata mema.

“Bibilia inasema tukikubali na kutii tutakula mema ya nchi, na sisi Tanzania na viongozi wetu tukitii tutakula mema ya nchi, tusipokubali na kutii, tunatengeneza mianya ya kuminya uhuru na kuleta vurugu katika nchi yetu.” Amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments