UFUNGUZI NA UWEKAJI WA MAWE YA MSINGI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO KUENDELA KESHO.

 

SHAMRASHAMRA za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kesho Disemba 27,2023 kwa uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi atazindua uwanja wa Amaani na miundombinu mengine ya michezo katika uwanja huo uliopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Massoud Othman anatarajiwa kufungua Skimu ya Masingini iliyopo Wilaya ya Magharibi “A”, huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kufungua kituo cha mama na mtoto Uzi Wilaya ya kati Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa atafungua tangi la maji safi na salama Unguja Ukuu wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Kwa upande wa Pemba Naibu Spika wa Baraza la Wakilishi Mhe. Mgeni Hassan Juma atafungua Soko la samaki na mbogamboga Machomane Wilaya ya Chakechake pamoja na kuweka jiwe la msingi ghala la chakula na vifaa vya ujenzi eneo la Kinyasini wilaya ya Wete Pemba.

Kutimiza miaka 60 ya mapinduzi kunaenda sambamba na kauli mbiu “miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar tuimarishe uchumi,uzalendo,na amani kwa maendeleo ya taifa letu.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments