Wananchi Musoma Vijijini wanashirikiana kujenga sekondari

WANANCHI wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema Wilayani Msoma wanajenga shule ya sekondari yao mpya wakilenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya elimu Musoma Vijijini.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ameieleza HabariLEO  kuwa shule hiyo itakayoitwa Muhoji Sekondari itakamilika na kuanza kutumika Januari, mwakani (2024).

“Ujenzi wa awali unaokamilishwa ni Vyumba 2 vya madarasa, Ofisi 1 ya walimu, matundu ya vyoo 12 ya wasichana, matundu 12 ya wavulana, matundu mawili ya walimu na barabara ya kuingia shuleni kutoka barabara kuu,” alisema.

Prof Muhongo alisema wachangiaji wakuu wa mradi huo ni wananchi wa Kijiji cha Muhoji, mbunge wa jimbo (yeye mwenyewe), mfuko wa jimbo, wazaliwa watatu wa Kijiji cha Muhoji.

alisema hata hivyo halimashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini mpaka sasa bado haijachangia.

“Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeombwa isaidie ukamilishaji wa ujenzi wa barabara linaloingia Muhoji Sekondari likitokea barabara kuu la Murangi- Masinono-Manyamanyama (Bunda).”alisema.

Prof Muhongo alisema Muhoji Sekondari itakuwa ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne ambavyo ni Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji.

Alisema Sekondari moja ya Bugwema Sekondari kwa Kata iliyopo sasa haitoshi kutokana na matatizo umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya wanafunzi na mrundikano madarasani.

Aliomba wadau wengine wa maendele wachangie ujenzi wa shule hii kwa lengo kuleta maendeleo ya elimu Musoma Vijijini na nchini kwa ujumula.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments