Watu 118 wafa kwa tetemeko China

WATU 118 wamekufa na wengine 182 kujeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jimbo la Gansu Maskazini Magharibi mwa China usiku wa kuamkia leo.

Umeme, maji, usafiri na mawasiliano vimekatika katika baadhi ya maeneo kutokana na tetemeko la hilo la kipimo cha 6.2, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Tetemeko hilo lilitokea katika jimbo linalojiendesha la Jishishan la Gansu, ambalo liko karibu na mpaka na Mkoa wa Qinghai ambapo nyumba 4,782 zimebomolewa.

Katika jimbo la Gansu waliokufa ni 105 na 397 wamejeruhiwa , mamlaka ya jimbo hilo ilieleza katika taarifa kwenda kwa waandishi wa habari asubuhi ya leo.

Mchanganuo wa waliopoteza maisha katika eneo la Qinghai ni 13 na 20 hawajulikani walipo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments