LICHA ya sare ya leo, kimahesabu klabu ya Yanga bado ina nafasi ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika endapo itashinda michezo miwili ya nyumbani na kupata sare Misri.
Sare ya bao 1-1 ya leo inaifanya Yanga kuwa na pointi 2, katika msimamo wa kundi D, Al-Ahly wanaongoza kwa pointi 5, CR Belouizdad pointi 4, Medeama 4.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, wamebaki na michezo mitatu, mchezo ujao watacheza na Medeama uwanja wa Mkapa, endapo Yanga itashinda itakuwa na pointi 5, kisha itasafiri kwenda Misri endapo itashinda au kutoa sare itakuwa na pointi 6-8.
Hesabu zitakamilika katika mchezo wa mwisho dhidi ya CR Belouizdad uwanja wa Mkapa endapo Yanga itashinda itakuwa na pointi 9-11.
Wakati Yanga inapiga hesabu hizo itaangalia pia na matokeo ya michezo mingine.
0 Comments