KLABU ya Yanga imfanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wake dhidi ya Medeama katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.Katika mchezo huo ambao Yanga imepata ushindi wa wa mabao 3-0, mchezo ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ili kufufua matumaini ya kufuzu Robo Fainali.
Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na kiungo wao nyota Pacome Zouzou, bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Medeama ilipata bahati ya kupata faida ya mkwaju wa penati mara baada ya mshambuliaji wao Sowah kuchezewa rafu na mlinzi wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto lakini penati haikuzaa matunda kwao kwani Kipa wa Yanga Djidji Diara kufanikiwa kuokoa mkwaju huo wa penati.
Mabao mengine ya Yanga yamefungwa kipindi cha pili na Bakari Mwamnyeto pamoja Mudathir Yahya.
Yanga Sc sasa itakuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na Al ahly ya Cairo.
0 Comments