Yatima kujengewa nyumba

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amejitolea kujenga nyumba kwa ajili ya watoto wawili waliofiwa na mama yao aliyeangukiwa na nyumba kutokana na mvua zilizoambatana na upepo mkali.
Mwishoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba 5, 2023 mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ilileta athari kubwa kwa wakazi 259 wa mitaa mitatu ya Kata ya Mbabala na kuwasabishia hasara kubwa ya mali ikiwemo upotevu wa mifugo na kupelekea kifo cha mama huyo Rahel Nguselo.
Rahel alipoteza maisha baada ya nyumba yake kubomoka na kumuangukia akiwa amelala na watoto wake hao wawili wadogo wa darasa la kwanza.
Mavunde ametembelea familia hizo zilizoathirika na kuahidi kuwajengea nyumba watoto hao ambao wamekosa makazi baaada ya nyumba yao kubomoka na kumuua mama yao.
Aidha, ametoa msaada wa mahindi tani 2 kwa waathirika pamoja na mahindi, magodoro, sukari, maharake, na maji katoni 100.
Kwa upande wa Mtendaji wa Mtaa wa Nguji-Mbabala Jumanne Misanga Njiku ametoa pole kwa wananchi wote waathirika kwa kadhia hiyo kubwa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa kama ambavyo imetabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Aidha,Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba ametoa pole kwa waathirika wa majanga hayo ya mvua na kuendelea kusisitiza juu ya kuchukua tahadhari kwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbalimbali ya nchini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments