Ahmed Ally: Wala msijikie unyonge wanasimba

BANDARINI, Dar es Salaam: MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa wanyonge kwa kulikosa Kombe la Mapinduzi, kwani wamefaidika zaidi na michuano hiyo kuliko vile walivyopoteza.

Ally amesema hayo alipowasili katika Bandari ya Jiji la Dar es Salaam, akitokea visiwani Zanzibar na kikosi cha Simba kushiriki Michuano ya 18 ya Mapinduzi.

“Kulikosa kombe la Mapinduzi, tumepoteza kitu kidogo mno kuliko faida tuliyoipata,” amesema kiongozi huyo maarufu ‘Semaji’.

Aidha, amezungumzia hali ya kikosi chao na kusema kama si leo basi kesho kuna wachezaji watakaoachwa kikosini na wale waliokamilishiwa uhamisho wao wa kuingia kikosini.

“Kabla ya tarehe 15, kila mmoja atafahamu hatma yake kabla dirisha halijafungwa.” Amesema Meneja huyo.

Ahmed hakusita kuzungumzia kuimarika kwa kiwango cha kiungo wa klabu hiyo, Fabrice Ngoma ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Mapinduzi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments