DC Agiza Maji Ya Visima Yapimwe

 

KATAVI; Mpanda. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za afya na maji kushirikiana, ili kuainisha idadi ya visima vilivyopo ndani ya wilaya hiyo na kuvipima kubaini maji ya visima hivyo yana usalama kiasi gani kwa matumizi ya binadamu.

DC Jamila ametoa maagizo hayo katika kikao kazi maalum cha kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mpanda.

Amesisitiza kila kaya kuhakikisha inazingatia suala la usafi wa mazingira, ikiwemo kunawa maji tiririka sanjari na kuwataka watumishi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kuweka nguvu kazi katika kutunza mazingira, hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Amewataka maofisa afya kufanya ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma ya chakula, stendi za mabasi na maeneo mengine yanayohusisha mkusanyiko wa watu, ikiwemo maeneo ya mabucha ili kuhakikisha udhibiti unaimarishwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments