Dk Mwinyi atunuku Nishani 17

IKULU, Zanzibar: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amewatunuku Nishani watunukiwa 17 ambao ni viongozi, askari na wananchi. Miongoni mwao wanne wameshafariki na 13 wangali hai.

Nishani zilizotolewa ni pamoja na Nishani ya Mapinduzi, Utumishi uliotukuka, Utumishi wa muda mrefu na Utii kwa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Nishani ya Ushujaa.

Hafla ya utunuku wa nishani hizo umefanyika leo katika viwanja vya Ikulu Zanzibar ikiwa ni sehemu ya sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, mwaka 1964.

Aidha, Rais Mwinyi amemtunuku Nishani ya Mapinduzi yenye sifa za kipekee ‘Order of praise’ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.

.

Vilevile miongoni mwa waliotunukiwa ni pamoja na Dk Mohamed Gharib Bilal, Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Seif Ali Idd, Marehemu Seif Shariff Hamad, Dk Abdulhamid Yahya Mzee, Prof. Saleh Idris Muhammed, Salum Faki Hamad, K0743 MCPO 1 Mohamed Suleiman Haji, K0694 MCPO1 Mohamed Salum Msellem, Lt.Col(Mst) Maryam Kurwa Nassor, Lt.Col. Seif Omar Makwega, Lt.Col. Khadija Ahmada Rai, Marehemu K1296S/1 Ramadhan Khalfan Ngozoma, Marehemu K0978 S/1 Ikrab Mikidasi Hassan, Marehemu Khalid Abass Hassan, Dk.Suleiman Maulid Mussa.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyombo vya ulinzi na usalama, Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments