Mshambuliaji wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa ameanza kwa kishindo safari ya kucheka na nyavu katika urejeo wake mpya ndani ya kikosi hicho baada ya leo kuiongoza timu yake kufanya maangamizi kwa Alliance Girls kwa kuibugiza mabao 7-0 katika mwendelezo wa Ligi kuu ya Wanawake.
Shikangwa amefunga mabao matatu katika mchezo huo na hivyo kutuma salamu kwa wapinzani wa Simba Queens juu ya uhatari wa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo wakati ligi inaanza ilikuwa ikiongozwa na Aisha Mnunka lakini ujio wa Shikangwa unaifanya Simba kuwa na safu hatari zaidi ya ushambuliaji.
Huu ni mchezo wa tatu kwa Shikangwa baada ya kurejea kikosini hapo wiki mbili zilizopita.
Mabao mengine ya Simba Queens yamewekwa nyavuni na Aisha Djafar aliyefunga mawili, Aisha mnunka aliyetupia moja huku Vivian Corazone akipigilia msumari wa mwisho.
Kwa matokeo hayo @simbaqueensctz imefikisha alama 16 baada ya kushuka dimbani mara sita wakifuatiwa na Jkt Queens yenye alama 15 katika michezo mitano.
0 Comments