Ihefu Fc mambo ni Moto Mkoani Arusha..

Klabu ya Ihefu Fc kwa sasa ipo mkoani Arusha ambako inaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa wakati huu ambao Ligi Kuu imesimama kupisha AFCON 2023.

Siku chache zilizopita wamiliki wa klabu hiyo walitangaza kukaribisha wadau mbalimbali kukaribishwa kuongeza nguvu kwenye timu hiyo.

Inaripotiwa kuwa klabu tayari imepata mdau ambaye ameweka mzigo wa kuinunua timu hiyo na mipango ya mdau huyo ni kuihamishia timu mkoani Arusha kwa muda(Tayari Ihefu wapo jijini Arusha).

Mdau huyo tayari pia ameanza kushusha vyuma vya maana ambavyo mambo yakikaa sawa watawatangaza.

Mbali na habari njema ya klabu kumpata mdau pia inaelezwa kuwa Ihefu Fc wataachana na wachezaji wake wa kigeni ili kupisha usajili wa wachezaji wapya wa Kigeni.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments