MADIWANI NA WATENDAJI WASOMEENI WANANCHI MAPATO NA MATUMIZI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA amewataka Madiwani na Watendaji wa Kata kuwasomea Taarifa za Mapato na Matumzi Wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

NAKOMOLWA alitoa wito huo wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya UGHANDI Wilaya ya Singida Vijijini wakati wa kuadhimisha Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.

Alisema ni lazima Wananchi wasomewe Mapato na Matumzi ili kuondoa sintofahamu katika kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu.

Aidha alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza Miradi mbalimbali kwa kutumia Fedha nyingi hivyo ni muhimu Taarifa za Mapato na Matumzi ziwe wazi.

Katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, NAKOMOLWA amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua Fomu za kugombea nafasi mbalimbali.

Alisema wakijitokeza kwa wingi na wakachaguliwa kwenye nafasi mbalimbali itasaidia Wanawake kushiriki katika ngazi zote za maamuzi zinazofanywa serikalini.

Pia aliwataka Wazazi kuhakikisha wanapinga Ndoa za utotoni zinazofanywa katika baadhi ya maeneo, na watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

NAKOMOLWA alisema kumuozesha mtoto ni kufanya kitendo cha Ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ambao wanatakiwa kusoma na sio kuwa Mama wa familia.

Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida ilifanya shughuli ya Upandaji Miti na Kuzungumza na Wananchi katika Kata UGHANDI, Wilaya ya Singida Vijijini, ikiwa ni moja ya shuguli zilizofanywa na Chama Mkoa kuelekea Maadhimisho ya Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM.







 Na RAFURU KINALA, Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments