Mambo safi Bandari Dar es Salaam

SHUGHULI za kiuendeshaji katika Bandari ya Dar es Salaam zinaendelea vyema huku gati zote ndani ya bandari hiyo zikiendelea na shughuli za kupakia na kupakua mizigo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Januari 28, 2024 na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho wakati akitoa ufafanuzi kuhusu madai ya uwepo wa msongamano bandarini kutokana na kutofanya kazi kwa baadhi ya gati.

Mrisho amethibitisha kuwa gati zote zinafanya kazi na kwa sasa meli zinaendelea kuhudumiwa katika gati zote.

Amesema leo pekee meli 13 kwenye gati zote kuanzia gati namba 0 hadi gati 11 zimeendelea kuhudumiwa na meli 31 zikiwa zinasubiri kuhudumiwa.

Mrisho ameongeza kuwa kwa upande wa gati za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), terminal l kuna meli zipatazo 10 zinaendelea kuhudumiwa ambazo zimebeba shehena mbalimbali

“Pale gati namba 0 kuna meli ya MV Yangze 32 inapakua, gati namba 1 kuna meli ya MV Loa Fortune inahudumiwa, gati namba 2
kuna MV African Macaw, huku gati namba 3 kukiwa kuna meli ya MV Tong Da na meli zote hizi zinapakua mizigo mchanganyiko” alisema Bw. Mrisho na kuongeza

“Gati namba 4 hivi sasa kuna meli ya MV Fearless, gati namba 5 kuna MV Anassa, gati namba 6 na 7 kuna MV MSC Nora III, pale KOJ I kuna meli ya MT NCC Abha, KOJ II kuna meli ya MT Lubersac na mwisho pale SPM kuna meli ya MT Torm Hannah ikiendelea kupakua.” Amesema.

Kwa upande wa gati za TPA terminal ll, ambazo ni gati namba 8,9 10, na 11, katika gati za TPA terminal ll, ambazo ni gati namba 8, 9, 10 na 11 hivi sasa Kuna meli tatu zikiendelea kuhudumiwa”

Ufafanuzi huo umetolewa, kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa, ni gati mbili pekee ndio zinazofanya kazi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kukamilika kwa sehemu ya miradi ya maboresho ya miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam kumeanza kuleta matokeo chanya kwani kupitia maboresho hayo kumekuwa na ongezeko la idadi ya shehena inayohudhumiwa kwa mwezi bandarini hapo.

Maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam yamehusisha ujenzi wa gati na uongezaji wa kina katika lango la kuingilia bandarini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments